Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Zhao Lijian amesema kuwa janga la virusi vya Corona limefika katika hatua ya kutisha na hivyo basi uamuzi wa Rais Trump wa kusitisha ufadhili katika shirika la afya duniani utaathiri mataifa yote duniani.
Marekani ndio mfadhili mkubwa wa WHO, ikichangia zaidi ya dola milioni 400 mwaka 2019 ambayo ni asilimia 15 ya bajeti ya shirika hilo la afya lenye makao yake Geneva.
Rais Donald Trump ameishutumu WHO kuficha ukweli kuhusu mlipuko wa virusi vya Corona na badala yake kuamini kila taarifa iliyotolewa na China kuhusu virusi hivyo.
Hatua hiyo ya Donald Trump imekosolewa vikali pia ndani ya Bunge la Congress nchini Marekani hasa na wabunge wa Democratic wengi wakisema kuwa uwamuzi huo haukubaliki na nikinyume na sheria ya Marekani na Unavunja Katiba ya nchi hiyo.
Naye spika wa bunge wa Nchi hiyo Nancy Pilosi amesema kuwa uwamuzi wa Rais Trump kwa WHO hauna maana yeyote.
Amesema dunia inaweza kushinda haya mampambano ya janga hili la Dunia(Corona) ikiwa tu kutakuwepo na ushirikiano wa pamoja wa Mataifa yote.