- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHAMA CHA UPINZANI NIGERIA CHAPINGA MATOKEO YA URAIS YANAYOTANGAZWA
Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria PDP kimesema hakitayatambua matokeo ya urais yanayotangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo ambayo yanaoonesha kuwa rais Muhamadu Buhari anaongoza dhidi ya mpinzani wake Atiku Abubakar.
Mwenyekiti wa chama hicho Uche Secondus amesema matokeo yanayoendelea kutangazwa hayakubali wala chama chake hakiyakubali.
Amedai kuwa Tume ya Uchaguzi ikishirikiana na chama cha rais Buhari cha PDP, kimebadilisha matokeo ya mwisho yanayowasilishwa katika kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo.
Akizungumza mfano wa matokeo ya jimbo la Nasarawa, kiongozi huyo wa PDP amesema, matokeo hayo hayafanani na yale yaliyotangazwa katika jimbo hilo.
“Matokeo yote yanayoendelea kutangazwa na Tume ya uchaguzi, sio sahihi na hayakubaliki na chama chetu, maafisa wa rais Muhammadu Buhari na chama cha APC wakishirlikiana na maafosa wa Tume ya uchaguzi wamejaribu kubadilisha mkondo wa historia kwa kubadilisha takwimu”, amesema Uche Secondus.
Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi (INEC) imesema matokeo yanayotangazwa ni sahihi na yanafanyika kwa wazi ili kila mmoja kufahamu kinachoendelea.
Katika hatua nyingine, Marekani kupitia ubalozi wake nchini Nigeria imetoa wito kwa wanasiasa dhidi ya kujitangazia matokeo na badala yake kutaka Tume kuruhusiwa kufanya hivyo.
Aidha, Marekani inataka wanasiasa kuheshimu mkataba wa kulinda amani waliotia saini mara mbili.
Ujumbe wa waangalizi wa Kimataifa waitaka Tume ya Uchaguzi Nigeria kuwa wazi
Waangalizi wa Kimataifa kuhusu Uchaguzi wa Nigeria, wametoa wito kwa Tume ya Uchaguzi kuwa wazi kipindi hiki matokeo ya urais yanapotangazwa na kuimarisha namna inavyowasiliana na umma na wadau wengine wa siasa katika chaguzi zijazo.
Aidha, wamesema ni vigumu katika ripoti zao za awali kusema iwapo Uchaguzi Mkuu nchini humo ulikuwa huru na haki kwa sababu mchakato bado haujamalizika, licha ya kusema kuwa zoezi la Uchaguzi lilifanyika kwa amani.
Ripoti za waangalizi hao pia zimebainisha changamoto mbalimbali zilizoshuhudiwa wakati wa kupiga kura Jumamosi iliyopita.