Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:38 am

NEWS: CHAMA CHA TALGWU CHAVUNJA UKIMYA KWA WANASIASA.

DODOMA: Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania TALGWU kimekerwa na baadhi ya wanasiasa kuwawajibisha na kuwadhalilisha watumishi wa Umma.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Uhusiano Kimataifa wa TALGWU, Shani Kibwasali Akisoma risala ya chama hicho wakati wa Mkutano Mkuu wa Kazi wa miaka miwili na nusu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(TALGWU)leo jijini Dodoma.

Shani amesema kitendo cha baadhi ya wanasiasa kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwadhalilisha na kuwaweka kana mahabusu wanachama bila sababu za msingi na kutozingatia sheria zinazowapa Mamlaka hayo ni kushusha heshima ya hadhi ,heshima na morali ya watumishi.

Ameendelea kusisitiza kwa kuitakakukemea vitendo hivyokwa kuwaeleza Viongozi wanasiasa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za masuala ya nidhamu kwa watumishi.

"Endapo italazimu mtumishi kuwekwa mahabusu kwa hofu ya uvunjifu wa amani basi matakwa ya kisheria yazingatiwe"alisema Shani.

Kero nyingine ni kukosekana kwa miundombinu na huduma za Msingi katika maeneo mapya yalipohamishiwa ofisi za Halmashauri ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Akiendelea kufafanua amesema watumishi wamehamishwa katika maeneo yao bila kuzingatia maandalizi ya kutosha, huku maeneo mengi hakuna majengo yenye hadhi ya Ofisi,huduma ya maji,huduma ya kijamii,usafiri,umeme,nyumba za kuishi pamoja na huduma nyingine za msingi.

Amesema pamoja na serikali kuwarejesha kazini wanachama waliodolewa kwa kukosa cheti cha ufaulu wa elimu ya kidato cha nne ambao waliajiliwa kabla ya Mei 20 mwaka 2004 na kuhaidi kulipa malumbikizo ya mishahara kwa miezi yote lakini yapata miezi 20 sasa hawajalipwa.

Mbali na hayo amesema baadhi ya wastaafu kutolipwa mafao yao kwa wakati jambo balo si jema kwa watumishi hao.

Naye Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akijibu risala ya Talgwu,amesema kuwa ni kosa kwa wanasiasa kuvuka mipaka kwa kuwawajibisha watumishi.

Amesema mwanasiasa anatakiwa kutambua mipaka yake ya kufanya kazi bila kuwadhalilisha watumishi na mtumishi anatakiwa kuwajibishwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi.