Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:59 am

NEWS: CHAMA CHA NCCR MAGEUZI KIMEJITOA UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA

Chama Kingine cha upinzania Nchini Tanzania Cha NCCR - Mageuzi kimetengaza hatua ya kujiondoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Image result for james mbatia nccr mageuzi

Mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia, ametangaza uamuzi huo leo mchana Jumapili Novemba 10, 2019 jijini Dodoma.

Chama hicho kinakuwa chama cha Tatu nchini hapa kujiondoa katika uchaguzi huo mara baada ya vyama vya Chadema , ACT-Wazalendo kufanya uwamuzi kama huo.

Sasa uchaguzi umekosa ushawishi kwakuwa vyama shindani vya Upizania nchini humo vimejitoa katika Uchaguzi huo.

Huenda taifa hilo likashuhudia idadi ndogo sana ya watu watakaojitokeza kupiga kura hapo novemba 24 mwaka huu.

''Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.'' Anasema Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT wazalendo katika mkutano na waandishi wa habari.

Zitto Kabwe ambaye ndio kiongozi mkuu wa chama hicho alitoa uwamuz huo mara baada ya chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema kutangaza kuwa kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi imesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ulivyopangwa tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu.

Ufafanuzi huo umetolewa mapema hii juzi katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni, Dodoma ambapo Mbunge wa Singida Kaskazini Justice Monko alitaka ufafanuzi wa serikali hasa baada ya Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kutangaza kujitoa rasmi katika mchakato wa Uchaguzi huo.