Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:50 pm

NEWS: CHAMA CHA DEMOCRATS CHAANZA MCHAKATO WA KUMVUA URAIS TRUMP

Washington: Wanasiasa watatu wa juu wa chama Cha Democrats wametoa wito leo wa kuanzishwa mchakato wa kumuondoa madarakani rais Donald Trump Saa chache baada ya aliyekuwa kiongozi wa timu ya wachunguzi kuhusu ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani Robert Mueller kusema kwamba uchunguzi walioufanya haukumfutia hatia rais Trump ya kukiuka sheria, akitofautiana pakubwa na matamshi ya Trump.

Image result for trump vs democrats senate

Akizungumza kwa mara ya kwanza Jumatano ya wiki hii, Robert Mueller kama kufafanua kile kilichomo kwenye ripoti yake, amesema suala la kumfungulia mashtaka rais aliyeko madarakani halikuwa ni suala lililoko mezani kwa wakati ule.

Mueller alikuwa amepewa jukumu la kuchunguza ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Suala la mchakato wa kumuondoa Trump madarakani limewagawa wabunge wa chama cha Democrats, ambapo baadhi wamejitokeza kuongeza shinikizo kwa spika wa bunge Nancy Pelosi, ambaye mpaka sasa hajakubali kuanzisha mchakato huo.

Matamshi ya Mueller sasa yamewaibua wagombea wengine watatu wanaoomba kuchaguliwa na chama chao kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, wakifanya idadi yao kuwa 10 ya wanaotaka mchakato wa kumuondoa Trump uanze.

Rais Trump kwa upande wake ameendelea kusisitiza kutokuwa na hatia akisema sheria zilizopo haziruhusu rais aliyeko madarakani kushtakiwa na hivyo mjadala wa Mueller umefungwa rasmi.