- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHAMA CHA BORIS JOHNSON CHASHIDA UCHAGUZI
Chama cha Conservative cha Waziri Mkuu wa Sasa wa Uingereza Boris Johnson kimeshinda Uchaguzi kwa zaidi ya Viti 326 ilivyokuwa inavinahitaji.
Johnson Amewashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Disemba.Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda zaidi ya viti 326, Boris Jonhson amesema kwamba hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.
Chama cha Boris Johsnon kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini kufikia sasa kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 334 wakati tukichapisha habari hizi.
Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Boris Jonson Jeremy Corbyn kusalimu amri na kusema kwamba hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Uamuzi huo wa kiongozi wa Leba unajiri huku chama hicho kikikabiliwa na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi katika miongo kadhaa.
Chama cha Conservative kimeshinda baadhi ya viti katika ngome za chama cha Leba.
Chama cha Leba kimepoteza viti kaskazini mwa England , Midlands na Wales yakiwa ni maeneo yaliopiga kura ya Brexit katika kura ya maoni ya 2016.