Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:48 pm

NEWS: CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAUJIA JUU UWONGOZI WA JPM

Leo chama cha ACT Wazalendo kimetoa 'Taarifa juu ya Hali Mbaya ya Upatikanaji, Usambazaji na Ugawaji wa Pembejeo kwa Wakulima wa Zao la Korosho Nchini'. Hali mbaya ambayo inatishia sekta nzima ya korosho nchini (zao linaloingiza fedha nyingi za kigeni kuliko mazao yote ya bishara nchini).

katika taarifa hiyo imesema kuwa Ili nchi kama yetu iendelee tunahitaji ukuaji wa kilimo (sekta inayoajiri 65.5% ya watanzania wote) kwa kiwango cha 10% kwa miaka mitatu mfululizo, kisha ukuaji wa 6% kwa miaka mingine 10.

ACT wamesema kuwa Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani ukuaji wa kilimo umedumaa zaidi, kwa mwaka jana kilimo kilikuwa kwa 0.6%, lakini uzalishaji wa korosho ulikuwa kwa zaidi ya 70%, ACT Wakapongeza wakulima wa korosho, hasa watu wa kusini,kuwa walilifuta machozi taifa, kwa kuingiza fedha za kigeni zaidi ya Dola milioni 340. "Inasikitisha sana kwamba Serikali sasa inataka kuwafukarisha, haithamini mchango wenu huu, alimalizia Edo shaibu (katibu wa itikadi na habari ACT wazalendo)