- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YATAKA JINA LA NEC KUBADILISHWA BAADA YA UWAMUZI WA MAHAKAMA
Mkurugenzi wa wa Mambo ya Nje, Mawasiliano, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mrema amesema wanapendekeza uwekwe utaratibu mpya wa kuteua wajumbe wa tume watakaosimamia uchaguzi nchini tofauti na huu uliopo sasa na hata jina la Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) kubadilika na kuwa TIEC.
“Uwekwe utaratibu mpya wa kuteua wajumbe wa tume, tunaweza tukafanya utafiti hapo Kenya utaratibu wa kuwapata wajumbe wa tume yao watu wanaomba, wanaangaliwa kwa vigezo na wanafanyiwa udahili, ukiangalia Ghana ipo hivyo hivyo , Afrika kusini hivyo hivyo ,tume hii isiitwe tena Nec bali iitwe TIEC,” Mrema alisema.
Mapendekezo hayo ya Chadema yametolewa Jana May 13, 2019 ambapo ni siku chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa hukumu iliyobatilisha uhalali wa wakurugenzi wa majiji, Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi nchini.
Uamuzi huo wa Mahakama ulitolewa Mei 10, mwaka huu kwa kubatilisha kifungu cha Sheria ya uchaguzi namba 7 (1) na 7(3) kinachoruhusu watendaji hao kusimamia uchaguzi.
Chadema kimepongeza uamuzi huo wa mahakama na kutoa mapendekezo saba
Akitaja mapendekezo mengine ni kuwapo kwa mfuko maalum wa tume hiyo, kuondolewa kwa zuio la kuishtaki tume mahakamani, matokeo ya urais kupingwa mahakamani, kura ya ndiyo na hapana pamoja na ushindi wa asilimia hamsini kwa wanaopita bila kupingwa na kuruhusiwa kwa mgombea binafsi.