- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YASUSIA UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA
Chama cha kikuu cha Upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimetangaza rasmi Alhamisi ya leo Novemba 7, 2019 kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakayofanyika November 24.
Chama hicho kinadai kuwa wakishiriki watakuwa wanahalalisha ubatili uliojitokeza katika zoezi zima la uchaguzi kuanzia uandikishaji, wapiga kura hadi wagombea kuwasilisha maombi ya kutaka kuwania nafasi za uongozi.
Awali vyama vya upinzani nchini humo vililalamikia mchakato wa wagombea wa nafasi mbali mbali wakiwashutumu wasimamizi wa uchaguzi huo kuhusika na njama za kuwaengua wateule wa vyama hivyo vya upinzani.
Vyama vya CHADEMA na Act Wazalendo ni miongoni mwa vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vikitoa malalamiko hayo kwa sehemu kubwa vikidai kuhujumiwa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika shughuli ya kuwapitisha wagombea wao.
Tumaini Makene ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA anasema kamati kuu ya chama chao ilikutana kujadili mustakabali wa uchaguzi huu na na hivyo kufanya maamuzi ya kuwa hakuna haja ya kushiriki katika zoezi ambalo lina dosari nyingi sana kiasi kwamba uchaguzi mzima hautakuwa huru na wa haki.
Act Wazelendo kinaeleza kuwa wagombea wao takriban elfu mbili wameenguliwa kugombea katika uchaguzi huo bila sababu za msingi