- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YAMPIGA MARUFUKU WAZIRI JAFO KUTUMIA JINA LAO
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempiga marufuku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo kuacha kutumia jina na nembo ya Chadema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu chama hicho kimejitoa na kimeondoa udhamini kwa wagombea wake.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Novemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam, na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Bara, John Mnyika akisema chama hicho kimejitoa kwa sababu ya dhuluma zilizofanyika kwenye mchakato mzima.
“Sisi kama chama tutamwandikia barua Waziri Jafo ya kumpiga marufuku kulitumia jina la Chadema au nembo yake katika mchakato wa uchaguzi kwa sababu tumejitoa,” amesema Mnyika.
Mnyika ametoa msimamo huo mara baada ya Waziri huyo wa Tamisemi leo kuruhusu wagombea wote waliochukua fomu za kugombea Uchaguzi wa serekali za Mtaa unaokusudia kufanyika Novemba 24 mwaka hu
u.Pia, amewataka wagombea waliopitishwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuendelea kuwasilisha barua za kujitoa kwa sababu ndiyo msimamo wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Amesema Kanuni ya 14 na 15 ya uchaguzi huo, inaelekeza mgombea wa uchaguzi lazima adhaminiwe na chama cha siasa, hivyo, kauli ya Jafo kuwatambua wagombea waliopitishwa ni upotoshaji.
Ametoa wito kwa wanachama wa Chadema na Watanzania kwa ujumla kupuuzia wito wa Waziri huyo na kutekeleza uamuzi wa Kamati Kuu ya chama yaliyofanyika Novemba 7, mwaka huu.