Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:31 pm

NEWS: CHADEMA YAITAKA NEC KUTOA SABABU KUKWAMA DAFTARI LA MPIGA KURA

Dar es salaam: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa ufafanuzi wa haraka kwa umma kuhusu kinachoonekana ni kukwama kwa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) katika baadhi ya maeneo, ikiwemo Halmashauri ya Chato, mkoani Geita, bila kuwepo kwa taarifa yoyote rasmi kwa umma.

"ni kwanini shughuli hiyo haijafanyika kwa kadri ya maelekezo ya ratiba ya uandikishaji" imesema sehemu ya taarifa.

Taarifa ya chadema iliyotelewa leo Sptemba 19, 2019 imesema kuwa Kwa mujibu wa barua ya Tume hiyo ya Juni 21, 2019 yenye Kumb. Na. EA/75/162/01A/158, iliyokuwa na kichwa cha habari, YAH; RATIBA YA UBORESHAJI YA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA, kutoka NEC kwenda kwa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi, pamoja na mambo mengine, iliwasilisha ratiba kamili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ambapo ilionesha kuwa uandikishaji katika maeneo ya Mkoa wa Geita (Halmashauri ya Chato), Mkoa wa Kagera na Mkoa wa Kigoma (kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mji wa Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Kakonko, Kasulu, Kibondo na) ulipangwa kufanyika Septemba 8, 2019 hadi Septemba 14, 2019.

"Shughuli hiyo haijafanyika hadi sasa, huku muda ukiwa umepita na hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa vyama vya siasa, wadau wengine wa uchaguzi na umma wa Watanzania kwa ujumla"

"Vile vile, vikao vya awali na vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kuapisha mawakala kwa Mkoa wa Kigoma (Halmashauri ya Uvinza), Mkoa wa Tabora, Katavi na Rukwa, bado havijafanyika kwenye halmashauri husika ili kujiandaa na shughuli ya uandikishaji iliyopangwa kuanza Septemba 21, 2019 hadi Septemba 29, 2019." imesema sehemu ya Taarifa hiyo

Kwamaana hiyo chadema,imeitaka NEC KUTOA sababu za kukwama kwa uandikishaji katika maeneo yaliyotajwa hapo juu ili kuondoa mtanziko kuhusu hatma ya uboreshaji wa DKWK katika maeneo hayo na mengine yanayofuata. Aidha, Chadema kinaitaka NEC kutoa taarifa rasmi kwa wadau iwapo kuna mabadiliko yoyote (mengine) ya ratiba ili waweze kujiandaa ipasavyo kushiriki hatua hiyo muhimu kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

"Chadema inaendelea kusisitiza wito wake kwa NEC kutambua unyeti wa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo kwa kuwa ratiba ya awali ilitangazwa kwa umma, ni wajibu wa Tume kuutarifu umma kuhusu mabadiliko yoyote ya ratiba yanapotokea na sababu za mabadiliko hayo, kwa sababu Watanzania wana haki ya kujua ili pia waweze kujiandaa kushiriki zoezi hilo." ilimalizia sehemu ya Taarifa hiyo