- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA WAMJIA JUU WAZIRI KANGI LUGOLA
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasi na Maendeleo Chadema wamemjibu vikali Waziri wa Mambo ya Ndani nchi Kangi Lugola, baada ya Jana Waziri huyo kumtaka Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kurejea Tanzania ili kusaidia upelelezi wa tukio lake la kushambuliwa na risasi jijini Dodoma.
Tanzania inakumbukumba ya Lissu kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mnao Septemba 7, 2017 Area D Dodoma nje ya nyumba aliyokuwa akiishi.
Jana Lugola katika mkutano wake na wanahabari jijini Arusha, alimtaka mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema), kurejea nchini kwa kuwa yeye na dereva wake ni mashahidi muhimu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa operesheni na mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kauli ya Lugola.
Amesema wanaotakiwa kufanya uchunguzi na kutoa majibu ya suala hilo ni Jeshi la Polisi.
Kigaila amesema kazi ya kukamata, kuchunguza na kufikisha mahakamani ni ya Serikali na kwamba Lugola alitakiwa kuwaeleza Watanzania nini Serikali imekifanya kuchunguza tukio hilo.
"Atuambie (Lugola) anamtaka Lissu arudi kwa document (nyaraka) gani ya kiofisi au anataka tuanze kufanyia kazi mambo ya mtaani,β amehoji.
Kigaila amesema kwa mujibu wa maelezo ya Lugola, Serikali haiwezi kuchunguza tukio ambalo mhusika yupo nje ya nchi, akibainisha kuwa kuna matukio mengi yamewahi kuchunguzwa wakati wahusika wakiwa hawapo.
"Wakati Lissu anapigwa risasi hao walinzi wa kampuni binafsi walikuwa wapi? Lugola awaeleze Watanzania hao anaowaita walinzi binafsi wanaolinda nyumba hizo walichukua hatua gani? Hao ndio walitakiwa kuwa wa kwanza kueleza,β amesema.