- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA WAILAANI SERIKALI KUPORO MALI ZA VIONGOZI WA CHAMA
DODOMA: UONGOZI wa Chama cha Demiokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati ,umelaani vitendo vya serikali kwa kuwapora mali viongzi wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati Alphonce Mbasa, amesema kitendo cha wanachama hicho kup[orwa mali zao au kuharibiwa mali walizonazo kinaonesha wazi kuwa ni kutaka kujenga chuki na kudidimiza siasa za upinzani.
“Tumekuwa tukishuhudia mara kwa mara viongzi wa Chadema wakiporwa mali zao au kuhariniwa mali walizonazo huku baadhi ya viongozi wa chama tawala wakiwa wanamiliki mali kama hizo lakini hakuna hatua yoyote ambayo inafanyika juu yao.
“Ni hivi karbuni mwenyeiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe alifanyiwa figisu katika jengo la Bilicanas,shamba lake la maua huko hai,kama hiyo haitoshi, tumeona mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Fredrick Sumaye kipolwa mali zake kwa madai kuwa hajaendeleza.
“Kama hiyo haitoshi hata mke wake amepolwa shamba kwa madai ya kutoendeleza je hapa tunatakiwa kujiuliza ni kwanini imekuwa kwa viongozi wa Chadema hali hii hii haiwezi kujenga afya nzuri ya vyama vya siasa na badala yake inaweza kusabisha chuki kati ya serikali na wanasiasa”alisema Mbassa.
Katika hatua nyingine ameitaka serikali kutochukua maamuzi ya kuwakomoa wanasiasa wa upinzani kwa maelezo kuwa vyama vya siasa vya upinzania vipo kwa muijibu sheria ya vyama vingi.
Mbassa amesema nchii hii kuna watu ambao wanamiliki mashamba mengi na hayaendelezwi, na kueleza kuwa wapo hata marais wastaafu pamoja na viongozi wengine.
“Tanzania ina eneo kubwa na ardhi kubwa hivyo viongozi wasidhani kuwapora wapinzania ardhi siyo utendaji bora bali ni kutengeneza chuki, ifike hatua serikali ikubali kukosolewabadala ya kufikiri kuwa atakaye ikosoa serikali hatanyanyaswa kwa kuumizwa katika kufirisiwa au kupolwa mali zao.
“Lazima tutambue kuwa tunajenga nchi moja kwa misingi ya amani, upendo na ushirikiano siasa zinazofanywa ziwe siasa za kujenga hoja na kutoa misimamo na mwelekeo ya nini kifanyike hatuwezi kunyamaza kwa kuogopa kufanyiwa vitisho ambavyo si salama kabisa.
“Kwa sasa tunashuhudia mambo mengi ya kuuminya upinzani mikutano ya adhara imekatazwa mikutano ya ndani pia nayo inafanywa kana kwamba haitakiwi mtu akitoka CCM na kuelekea upinzania anaonekana kama vile katenda dhambi jambo hilo linatakiwa kukemewa na kutopewa nafasi ili kuondokana na chuki ambazo zinaweza kujitokeza” alisema Mbasa.