- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA KUWAVUA UBUNGE WABUNGE WAO SABA
Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini kimepeleka mapendekezo kwenye kamati kuu ya chama hicho kuvuliwa nafasi za uongozi wa chama wabunge saba wa chama hicho na kuvuliwa uanachama kwa meya mmoja wa jiji kutokana na makosa ya kinidhamu ndani na Njee ya chama.
Mapendekezo hayo yametolewa baada ya kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho kukaa na kuamua kumvua uanachama Diwani Viti Maalumu Chadema katika jimbo la Arumeru Mashariki, Digna Nassari kwa tuhuma ya makosa ya kinidhamu na usaliti.
Taarifa ya Uwamuzi huo umetolewa jana Mei 22, 2019 na Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema chama hicho kina wabunge 14 na mameya wawili Kanda ya Kaskazini ambao baadhi wanashika nyadhifa za chama ikiwapo ujumbe wa kamati kuu, mawaziri vivuli na nafasi nyingine kadhaa.
“Viongozi hawa pia wametiwa hatiani kwa kukaidi kufika kweye vikao vya chama bila taarifa yoyote” alisema. Alidai baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakitoa lugha kwenye mikutano ya hadhara zinazokinzana na msimamo wa chama hicho.
Akitangaza uamuzi wa kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika Mei 18, mwaka huu na kuongozwa na kaimu mwenyekiti ambaye ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Golugwa alisema wamechukuwa uamuzi huo ili kukisafisha chama kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.
Kiongozi huyo hata hivyo aliomba kutotaja majina ya wabunge hao wanaopendekezwa kuvuliwa nyadhifa zao. Alisema tuhuma ambazo zimewatia hatiani viongozi hao ni kukaidi na kutoshiriki kazi za chama ambazo zinahitaji wao kutumia hadhi, heshima na uwezo wao ili kukijenga.
Golugwa alisema viongozi hao pia wametiwa hatiani kwa kukaidi maelekezo ya chama kuhusiana na michango yao kwa ajili ya ujenzi wa chama na utekelezaji wa maeneo waliyopangiwa ya kikazi ya Chadema.