- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CCM YAWATAKA MEMBE, KINANA NA MAKAMBA KUJIELEZA KWA UTOVU WA NIDHAMU
Mwanza. Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimewataka Makatibu wakuu wa zamani wa chama hicho Abdurhman Kinana na Yusufu Makamba waitwe na kuhojiwa katika Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.
Pia Halmashauri hiyo imemjumuisha mjumbe mwingine wa CCM, Benard Memb, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Njee wa Tanzania naye aitwe na kujieleza Juu ya Utovu wa nidhamu.
Maamuzi hayo yametolewa katika Kikao kilichokaa leo Ijumaa Desemba 13, 2019 jijini Mwanza chini ya Rais John Magufuli.
Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Katika mkutano huo, imewasamehe wanachama wake watatu huku wengine wakitwa kuhojiwa.
Walioitwa kuhojiwa ni makatibu wakuu wawili wa zamani wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na Benard Membe.
Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza.
Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 β 2030 sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Tanzania inayo ongozwa na Rais Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.
Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.
Wanachama hao ni;-
1. Ndg. Januari Makamba (Mb)
2. Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,
3. Ndg. William Ngeleja (Mb)
Kikao cha HKT kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.