Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:51 pm

NEWS: CCM MKOA WA DODOMA HAITAMVUMILIA MTOA RUSHWA.

DODOMA: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa amesema kamwe chama hakitamvumilia mtu yoyote atakayebainika kutoa au kupokea rushwa ili kushinikiza achaguliwe.


Akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT)Wilaya ya Dodoma Mjini Mkanwa amesema Kitendo hicho ni kinyume na kanuni na taratibu za chama.

Amesema Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt John Magufuli ameshaonyesha njia katika kupambana na rushwa,na wao viongozi wa chini yake ni lazima wamuunge mkono na kusisitiza yoyote atakayebainika atachukuliwa hatua.


“Niwapongeze viongozi wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini kwa jinsi mnavyochapa kazi na kuwa na msimamo imara katika kukemea na kuikataa rushwa kwa vitendo hongereni sana,”alisema Mkanwa.

Amewahimiza wanawake kujikita katika ajenda za maendeleo na zile zinazogusa maisha ya watoto kama vile lishe duni,kufuatilia masuala ya taaluma na mimba za utotoni.

“Pia ni lazima muhakikishe wanawake wa wilaya hii wananufaika na uwepo wa makao makuu yaserikali, pamoja na miradi mipya na mikubwa iliyopo kama stendi ya mabasi ile ya kisasa na soko,”alisisitiza Mwenyekiti huyo.


Amesema CCM Mkoa imeridhia kutoa kiasi cha Sh Milioni tatu kwa ajili ya kulipia gharama za kiwanja cha UWT wilaya ya Dodoma Mjini ambacho kitatumika kujenga vitega uchumi vya wilaya hiyo.

Aidha Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kutoa viti 100 na mahema,mbunge wa Viti maalum Felister Bura yeye amekabidhi viti 100 na kuahidi baadae kutoa mahema huku Fatma Toufiq ambaye ni mbunge wa viti maluum akiahisi kutoa mashine ya kudurufu(Photocopy Machine).

Kikao hicho kilipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Januari 2016 hadi Machi 2020 kutoka kwa madiwani wa viti maalum.