Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:49 am

NEWS: CAG AZUILIWA KUONGEA NA WAANDISHI BAADA YA KUHOJIWA

Dodoma: Hali ya sintofaham imejiri leo Jumatatu Januari 21 bungeni baada ya waandishi wa Habari kuzuiliwa kuzungumza na Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serekali CAG Prof. Mussa Asaad muda mchache Mara baada ya Kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge dhidi ya kauli yake "udhaifu wa Bunge"


Wakati CAG akiondoka saa 8:47 alitoka viwanja vya bunge, maofisa mbalimbali waliwazuia waandishi wa habari kumhoji chochote.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka, amesema kamati yake imemaliza kumhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na ametoa ushirikiano mkubwa mno.

CAG Assad aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba Mosi mwaka 2014 ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.

Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.