- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CAF YAMTAJA MANE KUWA MCHEZAJI BORA AFRICA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF Limemtaja mwanasoka bora wa mwaka 2019 kuwa ni Mchezaji wa CLUB ya Liverpool na Timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane.
Walioshiriki kinyang'anyiro cha tuzo hizo ni mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool -na wenzie walioshiriki kinyang'anyiro hicho ni mchezaji wa Misri Mohamed Salah na mchezaji wa Manchester City pamoja na winga wa Algerian Riyad Mahrez.
Mane ambaye ana umbaye ana umri wa miaka 27, aliweza kuisaidia Reds katika ligi ya mwaka 2018-2019 na kufunga magoli 30 katika msimu uliopita.
Aliweza kufunga magoli 15 mpaka sasa kwa mwaka 2019 mpaka 2020, na kuisaidia Liverpool kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 13.
"Nina furaha sana na ninajivunia kuwa mshindi. Kandanda ni ajira yangu ambayo ninaipenda," alisema Mane."Ninapenda kuwashukuru familia yangu, taifa langu , timu yangu ya taifa , wachezaji wenzangu, shirikisho na klabu ya Liverpool.Hii ni siku kubwa kwangu."
Mane alichukua tuzo yake katika sherehe zilizofanyika huko Hurghada, Misri.Lakini si Salah, ambaye alishinda tuzo hiyo mara mbili katika miaka miwili iliyopita wala Mahrez wali.
Mane alimaliza katika nafasi tatu za juu katika tuzo hizo katika miaka mitatu iliyopita.Na ilikuwa ni ndoto yake kushinda tuzo hiyo ili kufikia mafanikio ya shujaa wake El Hadji Diouf, ambaye alishinda mwaka 2002.