- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BWEGE ASIMAMISHA SHUGHULI ZA BUNGE KWA MUDA
Dodoma. Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Seleman Bungara maarufu kwa jina la Bwege leo Jumanne Juni 29, 2021 jina lake limemlazimisha Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson kusimamisha Shughuli za Bunge kwa muda kutokana na kushangiliwa sana na wabunge aliposimama kwa ajili ya kutambulishwa kama mgeni Bungeni.
Bwege ambaye sasa ni Mwanachama wa ACT Wazalendo aliyejizolea umaarufu katika mkutano wa Bunge uliopita kutokana na aina yake ya kuzungumza.
Bwege ametambulishwa na naibu Spika, Dk Tulia Ackson baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Dk Tulia alilazimika kutumia mamlaka yake kuwanyamazisha wabunge waliokuwa wakipiga makofi na meza.
Bwege alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi viwili kupitia CUF na alikuwa miongoni mwa wabunge maarufu kutokana na vituko vyake ndani ya Bunge.
Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 aligombea ubunge kupitia ACT- Wazalendo lakini akaangushwa na Francis Ndulane wa CCM ambaye alikumbana na maswahibu ya kushindwa kusoma kiapo alipoteuliwa kuwa naibu Waziri wa Madini.
Leo Bwege ametambulishwa bungeni kama mgeni wa mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda na alipotoka aliongozana naye.
"Wabunge basi inatosha ngojeni kwanza nitamtabulisha vizuri, inatosha wabunge subirini nitambulishe vizuri," amesema.
Kuhusu jina la Bwege, Dk Tulia amesema awali lilikuwa na shida kwa wapiga kura lakini baadaye walikubaliana nalo baada ya kuona limempa umaarufu mhusika