Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:43 am

NEWS: BURUNDI YAFUNGIA CHOMBO CHA HABARI CHA REDIO KWA UKOSOAJI

Bujumbura Kituo maarufu cha Redio nichi burudi CCIB FM+ kimefungiwa kwa muda baada ya kuikosoa serikali kufuatia mauaji ya warundi wakimbizi nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.

CCIB FM+, cha nchini Burundi mapema mwezi huu kilitoa taarifa za kukosoa mwenendo wa serikali baada ya mauaji ya warundi 36 katika maandamano ya sept 15 nchini Drc ambayo pia askari mmoja wa Drc aliuawa.

Mkurugenzi na muhariri Eddy Claude Nininahazwe aliiambia AFP kuwa kituo kimezuiwa kwa kutangaza ukimya wa serikali baada ya mauaji ya warundi.

Katika taarifa ya serikali baraza la habari lilidai kituo hiko kimefanya ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya habari na sheria zinazosimamia vyombo vya habari na kukiamuru kuzima mitambo yake kwa miezi mitatu kuanzia jumatatu.

Nininahazwe amelaani hatua hiyo akijitetea kituo chake hakikuvunja sheria yoyote.