- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE: UZEMBE WA WAENDESHA BAJAJI WACHANGIA ONGEZEKO LA AJALI
DODOMA: BUNGE limeelezwa kuwa sababu kubwa ya kutokea kwa ajali zinazohusisha Bodaboda na Bajaji ni uzembe wa baadhi ya waendesha Pikipiki kwa kutofuata sheria na kanuni za usalama barabarani.
Hayo Yameelezwa bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la Mbunge wa Chonga,Mohamed Juma Khatibu (CUF)
Khatibu amedai kuwa kumekuwa na wimbi kubwa lenye kutisha la ajali za bodaboda nchini kiasi cha kufanya hospitali zetu kupungukiwa na uwezo wa kuwahudumia waathirika wote wa jail hizo.
‘’Je Serikali inaweza kulieleza Taifa sababu za kutokea kwa wingi ajali hizo’’
‘’Je Serikali imejipanga kukabiliana na utiriri wa jail hizo bila kuathiri ajira hizo za bodaboda’’amehoji Khatibu.
Akijibu maswali hayo,Mwigulu amesema Pikipiki za matairi mawili(Bodaboda) na Matairi matatu (Bajaji) zilianza kutumika mwaka 2008 kubebea abiria na mwaka 2009 Bunge liliridhia vyombo hivyo vitumike kutoa huduma za usafiri wa abiria.
‘’Sababu kubwa ya kutokea kwa ajali za barabarani ni uzembe wa baadhi ya waendesha Pikipiki kwa kutofuata sheria na kanuni za usalama barabarani’’amesema
‘’Kama ambavyo nimekuwa nikijibu hapa bungeni serikali inatambua biashara inayofanywa na Pikipiki za kubeba abiria na inathamini mchango wao katika kutoa huduma hiyo ambayo imesaidia katika kurahisisha usafiri na kutoa ajira’’amesema
Amesema katika kukabiliana na ajali zinazohusu bodaboda Serikali kupia Jeshi la Polisi imekuwa ikichukua hatua dhidi ya waendesha pikipiki ambao hawazingatii sheria ya usalama barabarani pamoja na kanuni zake.
Pia amesema Jeshi la Polisi limekuwa likitoa mafunzo kwa waendesha bodaboda juu ya matumizi bora ya barabara