Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:17 pm

NEWS: BUNGE TANZANIA LAKATAA KUFANYA KAZI NA CAG

Dodoma: Katika hali isiyo ya kawaida, nchini Tanzania leo imeandika historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Maamuzi ya Bunge yamepitishwa leo Jumanne Aprili 2, 2019 baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka kuwasilisha na kusoma bungeni taarifa ya kamati hiyo iliyomhoji CAG, kumtia hatiani baada ya kubaini kauli aliyoitoa kuwa Bunge ni dhaifu, amelidhalilisha Bunge.

Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alitoa nafasi kwa wabunge kujadili jambo hilo huku wabunge wakipishana maoni yao, kukubaliana na uamuzi huo na wengine kupinga akiwemo Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe. "Historia ambayo mnaiandika leo itawahukumu.Bunge mnajipa utukufu ambao ni wa Mungu pekee. Azimio mnalotaka kulifanya leo dhidi ya CAG mmeshalifanyia kaz''

''Mnataka kuwanyima watu haki na uhuru wa mawazo ilhali Katiba imeruhusu kila mtu, akiwamo CAG ana uhuru wa kutoa mawazo na kueleza fikra zake, kufanya mawasiliano na kutoingiliwa kuhusu taarifa yake.'' amesema Mbowe ''Mkiendelea kuiongoza kamati hii ya maadili kama ilivyo sasa, umma utaona kamati hii ni mali ya chama. ''

Baada ya wabunge kutoa maoni yao, Dk Tulia amelihoji Bunge kuhusu hoja hiyo, akiwakata wanaokubaliana na jambo hilo kusema ndio na wasiokubaliana na suala hilo kusema sio, "waliosema ndio wameshinda. "