- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE LAPOKEA WITO WA KUSITISHA AZIMIO LA KUTOFANYA KAZI NA CAG
Dar es salaam. Tangu Bunge lipitishe azimio lake la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serekali (CAG) Prof Mussa Asaad kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi na viongozi mbali mbali juu ya uwamuzi huo, sasa kampeni ya mtandaoni iliyokusanya sahihi za wananchi zaidi 15,000 kupinga azimio la Bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Assad waraka wa kampeni hiyo umefikishwa katika ofisi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai jana mchana na muda mfupi ofisi ndogo hiyo ya Bunge ilikiri kupokea waraka huo " ni kweli wameleta na tumepokea lakini si unajua sisi hatuna chochote cha kusema ila atafikishiwa Mh Spika kama sio kesho basi kesho kutwa" alisema mmoja wa Maafisa wa ofisi hiyo ya Bunge
Waandaaji wa kampeni hiyo ambao ni Taasisi ya Change Tanzania wamesema jana Jumatatu Aprili 8, 2019 kuwa maoni hayo yaliyokusanywa yamefikishwa ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam na mengine yakitarajiwa kutumwa jijini Dodoma kuanzia kesho Jumanne.
Mratibu wa maoni hayo Msabaha Hamza Msabaha amesema maoni hayo yanafikishwa leo(jana) mchana. “Tunapeleka katika ofisi ndogo za Bunge hapa Dar es Salaam na mengine tutayatuma kwa ofisi za Bunge Dodoma,” amesema wakati akiwa njiani kwenda ofisi za Bunge.
Kampeni hiyo iliyoanzishwa Aprili 3, 2019 siku moja baada ya Bunge kuazimia kutofanya kazi na CAG Profesa Assad, imelenga kukusanya sahihi za wananchi kutoka sehemu mbalimbali kupinga hatua hiyo.
Wengi waliochangia maoni yao kwenye mtandao wamekuwa wakielezea namna walivyo tayari kusimama bega kwa bega na Profesa Assad. Wengi wanataka Bunge liendeshe mambo yake kwa kuzingatia matakwa ya kikatiba.
Wiki iliyopita Bunge la Tanzania lilipitisha azimio la kutofanya kazi na CAG baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za kudharau chombo hicho. Wabunge wamefikia uamuzi huo baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutaka waridhie mapendekezo yao dhidi ya CAG. Kamati hiyo ilimhoji CAG Januari 21 baada ya kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York mwezi Desemba 2018 ambapo alisema kuwa Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo Serikali.
CAG mwenyewe kupitia TBC alilithadharisha sana bunge kuwa suala hilo linaweza kuwa kubwa kuliko lilivyo sasa na kutaka busara itumike zaidi ili kupata ufumbuzi. "Tunaweza kuwa na mgogoro wa kikatiba, kwamba ripoti (za ukaguzi wa mwaka 2017-18) zimeshawasilishwa kwa Rais na mimi siwakilishi ripoti Bungeni, basi Rais atazipeleka ndani ya siku sita kama Bunge likikataa kuzipokea hilo ni tatizo kubwa zaidi. Ni dharau (kwa katiba) wasiwasi wangu ni huo. Zikiwasilishwa bungeni zinakuwa mali ya umma na mimi napata nafasi ya kuzungumza, na hilo pia linaweza kuwa tatizo. Tafsiri ya kuwa (Bunge) hatuwezi kufanya kazi na CAG ni tafsiri pana sana na inatakiwa