Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:30 pm

NEWS: BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA RELI YA MWAKA 2017

DODOMA: Bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya Reli wa mwaka 2017 huku serikaliikisema kuwa kupitia muswada huo utawezesha kutungwa kwa sheria itakayoanznisha shirika la reli Tanzania TRC ambalo litakuwa na jukumu la kuweka mfumo madhubuti wa utoaji huduma bora ya usafiri wa reli.

Ni katika vikao vya bunge la 11 linaloendelea hapa mjini Dodoma ambapo pamoja na shughuli bunge limepata fursa ya kujadili na kupitisha muswada wa sheria ya reli wa mwaka 2017 muswada ambao unatajwa kuwa mkombozi wa kutatua matatizo sugu yanayoikabili sekta ikiwemo miundombinu

Akiwasilisha hoja ya kupitishwa kwa muswada huo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa amesema kuwa kumekuwa na matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta ya reli nchini hivyo muswada huo utakuwa mwarobaini wa kutoa huduma nzuri


Seleman Moshi Kakoso ni makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Miundombinu akiwasilisha maoni ya kamati hiyo amesema kuwa kamati inaishauri serikali kuangalia kwa umakini swala la maslahi kwa wafanyakazi wa reli.

Baadhi ya wabunge waliopata fursa ya kuchangia juu ya muswada huo wamesema kuwa kufuatia muswada huo serikali ihakikishe inaweka ulinzi madhubutu wa miundombinu ya reli ambayo wakati mwingine baadhi ya wananchi wamekuwa wakiharibu miundombinu na wengine kuvamia.

Aidha katika hatua nyingine spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuzalilisha muhimili wa bunge hakivumiliki .

Reli ya Tanganyika pia Reli ya Kati ilikuwa jina la njia ya reli kuanzia Dar es salaam kwenda Kigoma kwenye ziwa la Tanganyika ilijengwa katika miaka 1905 hadi 1914 na wakoloni