Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:20 pm

NEWS: BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA MADAKTARI .

DAR ES SALAAM: Bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya madaktari,madaktari wa meno na wataalamu wa Afya shirikishi ya mwaka 2017 huku serikali ikitoa hofu kwa madaktari wasaidizi na madaktari wasaidizi wa meno kuwa muswada huo haukusudii kufuta leseni za.

Madaktari wa meno wanasimamiwa na sheria ya mwaka 1953 sura 152 licha ya uwepo wa sheria hii kumekuwa na changamoto katika kukidhi mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo kupitia muswada huo utawezesha kukidhi mabadiliko hayo na kuitambua sekta ya madaktari,madaktari wa meno na wataalamu wa Afya

Akiwasilisha hoja ya kupitishwa kwa muswada huo bungeni mjini Dodoma Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na salama.

Akiwasilisha maoni ya kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii kuhusu muswada huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Peter Serukamba amesema kuwa kuna kila sbabau ya wanatalaama wa fani hiyo kuendelezwa na kupewa Bima ya Madaktari

Kwa upande wake msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu wizara hiyo Dkt Godwin Mollel amesema kuwa kupitia muswada huo uhakikishe unadhamini na kutambua mchango wa wataalamu hao wa sekta ya Afya.

Baadhi ya wabunge wakichangia maoni juu ya muswada huo wamesema kupitia utawezesha sekta ya madaktari wasaidizi pamoja na madaktari wa meno kutambulika na itasaidia kuongeza ufanisi kwa watendaji.

Idadi ya madaktari na madaktari wa meno waliosajiliwa hadi sasa ni 6077,madaktari wasaidizi na madaktari wa meno ni 3326,matabibu na matabibu wa meno ambao hawajasajiliwa wanakadiriwa kufikia 6170

Hata hivyo Bunge linataraji kuahirishwa hapo kesho Sept 15 mwaka huu