Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:40 pm

NEWS: BUNGE LAMTAKA LUGOLA KUTOA MAELEZO KUHUSU SAKATA LA UFISADI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Nagenjwa Kaboyoka, amemtaka alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola kutoa maelezo ya KINA kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini Tanzania.

Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo. “Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.

Mwenyekiti huyo wa PAC amemtaka Lugola, aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo. “Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.

Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo. “Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.

“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa.

Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni. Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo. “CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.

Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU. Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini Tanzania (TAKUKURU) imemuweka chini ya Ulinzi Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya ndani, kwa madai ya ufisadi,