- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE LAARISHWA SERIKALI YALAANI MATUKIO YA KUSHAMBULIWA KWA VIONGOZI
DODOMA: Waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ameahirisha shughuli za bunge mjini Dodoma huku akidai kuwa serikali inalaani matukio ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa viongozi na wananchi mbalimbali yanayoendelea nchini na kuwataka wananchi na wabunge kuwa watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya uchunguzi.
Ni katika siku ya mwisho ya kuahirisshwa kwa shughuli za bunge mkutano wa nane wa bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania hapa mjini Dodoma ambapo kabla ya kuahirishwa kwa shughuli za bunge,wabunge walipata fursa ya kushiriki kipindi cha maswali na majibu
Waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amesema serikali haitavumilia matukio hayo yanayohatarisha amani ya nchi na hivi sasa vyombo vya ulizi na usalama vinawasaka wahusika na kuwakamata hivyo wabunge na wananchi waviache vyombo hivyo vifanye kazi yake.
Pia waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo.
Katika hatua nyingine Spika wa bunge Job Ndugai amewataka wabunge pamoja kuwa makini na usalama wao huku akiwataka wananchi kuwa makini na watoto wao kulingana na matukio yanayoendelea hivi sasa nchini.
Awali kabla ya hoja ya kuahirisha bunge mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya ulinzi na usalama iliyotakiwa kuwasilisha taarifa kuhusu hali ya usalama kwa wananchi na wabunge Adadi Rajabu ameomba kupewa muda zaidi ili kumaliza kazi hiyo na kuiwasilisha bungeni.
Bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limeahirishwa mpaka tarehe 7 Nov litakapokutana tena hapa mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli za kibunge