Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:27 am

NEWS: BUNGE LA ULAYA LAIWEKEA TANZANIA VIKWAZO

Wabunge wa Bunge la umoja wa Ulaya kwa kauli moja wamekubaliana kuifutia Tanzania misaada na mikopo yote ambayo iliombwa na ilisainiwa na Umoja wa Ulaya (EU) na mashirika yake.

Bunge hilo limefikia uamuzi huo hii leo Novemba 19, 2020 kutokana na madai ya Ukiukwaji wa demokrasia kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Pia vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu vinavyodaiwa kufanywa na vyombo vya dola.

Tukio lingine ni madai kwa Serekali ya Tanzania kushindwa kudhibiti matukio ya ugaidi kusini mwa Tanzania(Lindi na Mtwara)

Moja ya misaada mikubwa ambayo Tanzania itaukosa ni ule wa £626M (sawa na TZS Trilioni 1.6) ambazo Tanzania imekuwa ikizipata kila mwaka tangu mwaka 2014 kwa ajili ya kuimarisha demokrasia, utawala bora, ujenzi wa miundombinu na kusambaza nishati ya umeme vijijini(REA).

Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya nje wa bunge la Ulaya (Chairman of the European Parliament Foreign Affairs Committee), David McAllister amesema pamoja na kuinyima Tanzania msaada huo wa TZS Trilioni 1.6 Pia umoja wa ulaya unafikiria kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi (Economic sanctions) ikiwa ni pamoja na kuizuia Tanzania kufanya biashara na nchi yoyote ya Ulaya sambamba na washirika wake.

McAllister amesema vikwazo hivyo vikiwekwa havitaondolewa mpaka pale serikali ya Tanzania "itakapojicommit" kwa maandishi kuheshimu demokrasia, kuruhusu ushindani wenye usawa wa vyama vya siasa na kulinda haki za binadamu.

Sambamba na hilo Bunge hilo limehoji fedha Euro milioni £27 ambazo Tanzania iliziomba katika umoja huo kwa lengo la kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

McAllister amehoji kuwa Tanzania imechukua kiasi hicho cha fedha huku Serekali ya nchi hiyo imeshatangaza kuwa nchi hiyo haina tena maambukizi ya Covid19, na Pia nchi hiyo ilishindwa kufuata masharti ya Msaada huo ukiwa ni pamoja na kutoa takwimu za ugonjwa huo na kushindwa kufuata muongozo uliowekwa na shirika la afya Duniani (WHO).