- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE LA MAREKANI LAMTAKA RAIS TRUMP KWENDA KUJIELEZA
Spika wa Bunge la baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi, amemtaka rais wa nchi hiyo Donald Trump kwenda kujieleza mbele ya baraza hilo na kueleza ukweli wake mbele ya kamati inayofanya uchunguzi dhidi ya rais huyo.
Seneta mwingine Chuck Schumer ambaye kama Pelosi anatoka chama cha Democratic, ameunga mkono wito huo, akisema ikiwa Trump hakubaliani na yanayosemwa katika mchakato wa kumchunguza, badala ya kutuma ujumbe wa twitter anapaswa kujieleza mbele ya kamati ya uchunguzi, tena chini ya kiapo.
Kupitia mtandao huo huo wa twitter, hivi punde Rais Trump amesema anafikiria kuitikia wito wa Pelosi na kujieleza mbele ya kamati inayomchunguza. Haya yanajiri wakati mchakato wa uchunguzi unaoweza kufungua njia ya kumshitaki Rais Trump ukiingia katika wiki ya pili, ukitarajiwa kumkaribisha mtu anayechukuliwa kama shahidi muhimu kuliko wote, ambaye ni balozi wa rais Trump katika Umoja wa Ulaya, Gordon Sondland.