Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:28 am

NEWS: BUNGE LA IRAQ LAPIGA KURA KUAYAONDOA MAJESHI YA MAREKANI

Bunge la Iraq limepiga kura hii leo ya kuyaondoa Majeshi 5,000 ya Marekani yaliyomo kila kona ya nchi Hiyo.

Wabunge hao wamepiga kura hiyo kupitisha azimio linaloitaka serikali kuviamrisha vikosi vya kijeshi vya kigeni kuondoka nchini humo mara moja.

Hatua hiyo imechukuliwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa leo.

Azimio hilo hasa linalenga kumaliza makubaliano yaliyoafikiwa mika minne iliyopita yaliyoiruhusu Marekani kutuma vikosi vyake vya kijeshi kusaidia katika vita vya kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislam IS.

Kura hiyo imepigwa siku mbili baada ya Marekani kumuua jenerali wa kijeshi wa Iran Qassem Soleiman akiwa nchini Iraq. Azimio hilo limeungwa mkono na wabunge wa madhehebu ya Kishia wenye mafungamano na Iran, ambao ndiyo wenye viti vingi bungeni.

Wabunge wa madhehebu ya Kissuni na wa kabila la Wakurdi hawakuhudhuria kikao hicho, ikisemekana kwamba wanaupinga mpango huo