- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Bunge kufutilia mbali huduma ya Obamacare Marekani
Marekani: Bunge la wawakilishi Marekani limepiga kura leo kufutilia mbali sheria ya huduma ya afya ya nafuu unaojulikana kama Obamacare.
Wanachama wa Republican wana imani kwamba sasa wana kura za kutosha.
Kevin McCarthy, kiongozi wa wengi bungeni amesema kwamba hatua muhimu imepigwa kuelekea kuidhinishwa mojawapo ya ahadi alizotoa Rais Donald Trump wakati wa kampeni.
Kipengee kilichokarabatiwa kinachoahidi dola bilioni 8 kusaidia watu walio na magonjwa ya kitambo, kinaonekana kuwaridhisha waliokuwa na shaka.
Jitihada ya awali kufutilia mbali sheria hiyo mnamo Machi haikufaulu na ilikuwa mojawapo ya wakati mgumu wa siku mia moja za kwanza za rais Trump katika utawala.