- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE KUENDELEA HADI JULY 5
DODOMA: SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai leo June 29 ametangaza kuongezwa kwa muda wa vikao vya Bunge kutoka june 30 hadi july 05 mwaka huu ili kuifanyia kazi miswaada mitatu ya sheria ya Serikali
Akitoa tamko la mabadiliko hayo Mh.Ndugai amesema miswaada hiyo ataipeleka kwenye kamati za kudumu za Bunge ili ifanyiwe kazi na utaratibu kama ipasavyo
Aidha Ndugai ameongeza kuwa kamati ya pamoja aliyoiunda itajumuisha kamati nyingine nne na kazi yake kubwa itakuwa ni kuchambua miswaada hiyo na kuandaa taarifa itakayowasilishwa Bungeni june 04 mwaka huu.
Kufuatia miswaada hiyo ratiba ya Bunge imebadilika na kuwa mkutano huu wa saba wa Bunge utaahirishwa siku ya july 05 mwaka huu