- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOSS TAKUKURU AKIRI KUTAFUNA PESA ZA UMMA
Dar es Salaam. Wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor umedai kuwa.
wameandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kukiri makosa yake .
Mansoor anakabiliwa na mashtaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha Sh1.477 bilioni.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu kuwa bado upelelezi haujakamilika.
Wakili wa Utetezi, Elia Mwingira amedai kuwa wameandika barua kwenda kwa DPP kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa, hivyo ni vyema kupata majibu kwa haraka ili mshtakiwa aweze kupata haki yake ya msingi.
"Tunaomba upande wa mashtaka kulifuatilia hili ili mteja wetu aweze kupata haki yake ya msingi," amedai Mwingira.
Baada ya maelezo hayo, Simon amedai kuwa suala hilo atalifuatilia kwa haraka na
Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya Agosti 13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku akijua kuwa si kweli.
Katika shtaka la pili, inadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017 huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshtakiwa kwa kudanganya, alijipatia Sh5.2 milioni kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru, kama malipo ya kiwanja kilichopo Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Pia, inadaiwa kati ya tarehe hizo, Mansoor alijipatia Sh3 milioni kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kuwa alijipatia Sh5milioni kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo.
Katika shtaka la tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh7 milioni kutoka kwa Ekwabi Majungu ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.
Mansoor anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa ofisi hiyo, alijipatia Sh7 milioni kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.
#mwananchi