- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOSI WA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI 'EL CHAPO' AHUKUMIWA MAISHA
Mlanguzi mkuu na sugu wa dawa za kulevya Duniani raia wa Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman, aliyepatikana na hatia ya kuendesha biashara ya kihalifu iliyosababisha vifo vya watu wengi na kuingiza nchini Marekani tani nyingi za dawa za kulevya, amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Jaji wa Marekani Brian Cogan ametangaza hukumu hiyo ya maisha pamoja na miaka 30, ambayo ni lazima chini ya sheria, katika kikao cha mahakama ya serikali kuu mjini Brooklyn.
Guzman mwenye umri wa miaka 62, pia aliamriwa kulipa dola milioni 12.6. Guzman alipatikana na hatia Februari mwaka huu kwa kusafirisha Marekani tani za cocaine, heroin na bangi na kuhusika katika njama za mauaji wakati akiwa kiongozi wa mtandao maarufu nchini Mexico wa biashara ya dawa za kulevya wa Sinaloa.