- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOSI WA HALOTEL AFIKISHWA MAHAKAMA KWA UTAKATISHAJI WA FEDHA BILIONI 78
Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel Son Nguyen (46), na vigogo wengine watano wa Viettel Tanzania wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78
Washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40) na Vu Tiep Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Mkuu Monica Mbogo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, imedaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26,2020 huko Mikocheni washtakiwa waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida.
Katila shtaka la pili ikidaiwa siku na mahali hapo na katika maeneo mengine ya nchi ya Tanzania washtakiwa kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA.
Imeendelea kudaiwa kuwa kati ya Julai 7,2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam washtakiwa kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu.
Aidha washitakiwa hao wanadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganisha Viettel Tanzania na Vietnam kinyume na sheria na pia wanadaiwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA ambapo waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75.
Katika shtaka la sita washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03 huku pia wakidaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu.
Aidha kampuni ya Viattel Tanzania ilitakatisha Sh bilioni 3.03 huku katika shtaka la tisa na 10, washitakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
Hata hivyo washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu ambazo kwa kawaida kusikilizwa mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande