Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:25 pm

NEWS: BOMBA LA MAFUTA KUAAJIRI ZAIDI YA WATU 10,000 NA KUGHARIMU DOLA BIL 3.5

Tanga: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Tanzania katika kijiji cha Chongoleni, Rais magufuli ameambatana na Rais wa Uganda Yuweri Museveni katika uzinduzi huo.

Rais Magufuli amesema kuwa bomba hilo litasaidia kupata mapato kwa sababu litatoa ajira kwa watu zaid ya 10,000 na litapita katika vijiji 124 na mikoa 8, mradi huu utasimamiwa na makampuni 3 na yatajenga matanki 5 kwa niaba ya kuhifadhia mafuta,

Mradi huu utagharimu dola za kimarekani Bilioni 3.5 na baada ya kujigwa kwa mradi huu unakusudia utaongeza wawekezaji kwa zaidi ya asilimia 55, Mradi huu umepangwa kuanzwa Januari 2018 na utachukua miaka 3 kuukamilisha.