- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BODI YA MIKOPO YAWATAKA WENYE VYETI FEKI KULIPA MKOPO
Dar es salaam: Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu Tanzania HESLB imewataka wafanyakazi wote walio tumbuliwa kwa sakata la vyeti feki kurejesha mikopo yao nakusema kuwa hata kwa waliofeli au na ambao hawakuendelea na masomo yao wanalazimika kurejesha mikopo, Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa HESB, Abdurazack Badru alisema kuwa kuna mafanikio waliyo yapata yametokana na hatua tatu kuu walizozichukua kuhakikisha marejesho ya mikopo yanafanyika, ambazo ni pamoja na kuwatafuta wadaiwa sugu wa kuanzia mwaka fedha 1994/95.
Badru alisema kuwa hadi sasa wamesha kusanya Sh 216,992,990,52.98 kati ya Sh 427,708,285,046.48 za mikopo ambayo ipo tayari kukusanywa. Pia imesema licha ya kuendelea kuwatafuta wadaiwa sugu 100,000 kwa sasa, marejesho iliyoyakusanya yameivusha kutoka kwenye lengo ililojiwekea katika mwaka wa fedha 2016/17 la kukusanya asilimia 40 ya mikopo yote iliyoiva. Pia Badru aliwashukuru waajiri (BOSS) wa sekta binafsi kama makampuni na taasisi zingine kwa kusaidia kukusanya kiwango kikubwa cha pesa kupitia wafamnyakazi wao,“Sekta binafsi nayo imetusaidia ingawa kundi la waliojiajiri mfano kuendesha bodaboda na wanaoendesha kilimo na ujasiriamali mwingine lenye wanufaika 28,893 nalo limerejesha jumla ya Sh bilioni 13.7 na kutuonesha mwitikio mkubwa zaidi,” alieleza.
Aliongeza kuwa bodi hiyo inapitia changamoto nyingi kukusanya marejesho ya mikopo iliyoitoa kwa sababu baadhi ya waajiri hawana taarifa zao zilizokamilika na sahihi huku wengine wakikata marejesho hayo kutoka kwenye mishahara na kutoyawasilisha kwenye bodi hiyo kwa wakati au kutoipeleka kabisa.
Alisema tayari imekwisha wafikisha mahakamani waajiri watatu ambao ni kampuni kwa makosa hayo ya kukaa na fedha za marejesho ya mikopo ilhali wamekwishayatoa kwenye mishahara ya wanufaika ambao ni waajiriwa wao. Kwa maelezo yake, hadi sasa wanawatafuta wadaiwa sugu 100,000.