Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:24 am

NEWS: BODI YA MIKOPO IMETOA ORODHA YA TATU YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini Tanznia (HESLB) imetoa orodha ya tatu ya majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mkopo yenye jumla ya wanafunzi 4,785 wa mwaka wa kwanza wa masomo 2019/2020.

Tokeo la picha la Abdul-Razaq Badru

Wanafunzi hao wamepata mikopo yenye thamani ya Sh14.3 bilioni na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo kufikia 46,838. yenye thamani ya sh162.86.

Orodha ya kwanza ilitolewa Oktoba 17 mwaka huu na ikiwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza 30,675 waliopata mikopo yenye thamani ya Sh113.5 bilioni huku orodha ya pili ikitolewa Oktoba 26 mwaka huu ikiwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza 11,378 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Sh35.06 bilioni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Novemba 3, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru imeeleza kuwa wanafunzi waliopata mikopo katika awamu ya tatu wanaweza kupata taarifa zao kupitia akaunti walizotumia kuomba mkopo Badru amesema majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo katika awamu hii ya pili yanapatikana katika mtandao wa HESLB wa uombaji mkopo (https://olas.heslb.go.tz) na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).