- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOBI WINE AFIKISHWA MAHAKAMANI, AKITUHUMIWA KUFANYA MAANDAMANO BILA KIBALI
Kampala: Jeshi la Polisi nchini Uganda linamshikilia tangu jana Jumatatu mwanamuziki na mbunge wa Kyadondo, Robert Kagulani maarufu kama Bob Wine na tayari amefunguliwa mashtaka ya kufanya maandamano bile kufata sheria.
Bob Wine alipandishwa kizimbani katika mahakama moja jijini Kampala na kusomewa mashtaka ya kuandaa mkutano na kufanya maandamano kinyume cha sheria mwaka 2018 na baadaye kuzuiwa katika Gereza la Luzira.
Mmoja wa wanasheria wa Bob Wine, Asuman Basalirwa amesema mteja wake amekamatwa kwa sababu za kisiasa.
Hata hivyo Serikali kupitia kwa naibu msemaji, Shaaban Bantaliza, anasema Bob Wine pamoja na watu wengine wanaopenda kuandamana bila kufuata sheria hawataachwa na mkono wa sheria.
Bob Wine anatajwa kuwa tishio kwa mustakabali wa siasa za rais Yoweri Kaguta Museveni.