- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BLOGA AENDELEA KUSOTA RUMANDE, UPELELEZI WA KESI YAKE HAUJAKAMILIKA
Upelelezi wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili Shamim Mwasha (41) ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion, hapa nchini na mumewe, Abdul Nsembo(45), haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mfawidhi, Kelvin Mhina, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutukwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine.
Baada ya kudai hayo, Wakili wa Utetezi, Charles Kisoka na Hajra Mungula, walidai kuwa shauri hilo halina dhamana, hivyo wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.
Wakili Wankyo alidai kuwa, amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2019 na washtakiwa walirudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.
Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.
Shamim na mumewe, wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei mosi, mwaka huu wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.