- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BINTI WA KUIBA KWENYE ATM KUFIKISHWA KORTINI
JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia mkazi wa Chalinze, Halima Juma (23) kwa tuhuma za wizi wa fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema Novemba 11 mwaka huu walimkamata Halima akiwa katika ATM za Benki ya CRDB tawi la Mbagala akijifanya kuwasaidia wazee.
“Halima alijifanya kuwasaidia wazee hasa wastaafu, wasiojua kutumia mashine hizo kwa lengo la kuchukua namba za siri na kuwabadilishia kadi na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao,” alisema Mambosasa.
Alisema alikuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiwabadilishia kadi zao halisi za benki na kuwapa nyingine na baadaye kuiba fedha zilizopo kwenye akaunti zao.
Alisema askari walimtilia shaka na kumkamata na baada ya kukaguliwa ambapo alikutwa na kadi 23 za benki kutoka kwa watu tofauti alizokuwa amezificha kwenye pochi aliyokuwa ameificha sehemu za siri.
“Tumemkuta na kadi za benki ya CRDB saba, NMB sita, NBC mbili, Amana mbili, Benki ya Posta mbili, ACB mbili, Stanbic moja, DCB moja na Equity kadi moja,” alisema Mambosasa.
Alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na jeshi hilo na atafikishwa mahakamani ushahidi utakapokamilika.