- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BINTI WA KIDATO CHA NNE AJIUWA KWA RISASI
Morogoro: Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Lupanga manispaa ya Morogoro, Jasmine Ngoye mwenye umri wa miaka 18 amefariki dunia baada ya kujipiga risasi,kwa kutumia bastola ya shemeji yake, chanzo kikielezwa kuwa ni msongo wa Mawazo aliokuwa nao kwa muda mrefu.
Inaelezwa kuwa kabla ya kujipiga Risasi binti huyo alimuachia ujumbe mfupi rafiki yake wakaribu aliyekuwa akisoma naye darasa moja.
Tukio hilo limetokea Jumanne Februari 19, 2019 eneo la Kola B mtaa wa Bogwa na mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa ukiwa na bastola pembeni aina ya Bereta ikiwa na magazini moja na ganda la risasi.Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Februari 21, 2019 Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema muda mfupi baada ya tukio hilo, shemeji wa binti huyo, Profesa Hamisi Mahigi alijitokeza na kueleza kuwa bastola hiyo ni yake na anaimiliki kihalali.
Kamanda huyo amesema binti huyo aliacha ujumbe aliouandika katika kitabu chake cha kumbukumbu kabla ya kujipiga risasi, alimkabidhi rafiki yake aliyekuwa akisoma naye darasa moja, Imelda Milanzi.
Katika kitabu hicho mwandishi huyo ameandika; “Ni mtoto asiye na wazazi wake na asiyejua kazaliwa wapi? Mtoto huyu anatamani kukiona kifo chake wakati wowote, mtu yeyote atakayesoma dayari (diary) hii ndiye atakayeandika siku ya kifo chake.”
Amesema profesa huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano. Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.