Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:52 am

NEWS: BINGWA WA NDONDI DUNIANI ANDY RUIZ JR AGOMA KUPIGANA SAUDIA

Mbabe wa Anthony Joshua ambaye ni Bingwa wa ndondi anayeshikilia mataji matatu katika uzani mzito zaidi duniani Andy Ruiz Jr amesema kuwa hajatia saini mkataba wa kupigana na Anthony Joshua nchini Saudia na kutumai kwamba pigano hilo litafanyika New York.

Image result for Andy Ruiz Jr

Mechi ya marudiano iliotarajiwa kufanyika Disemba 7 nchini Saudia ilitangazwa siku ya Ijumaa na promota wa Joshua - Eddie Hearn aliambia mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatano kwamba makubaliano yameafikiwa.

Image result for Andy Ruiz Jr

Ruiz hakuzungumzia kuhusu pigano hilo ama hata kuchapisha katika mitandao ya kijamii hadi siku ya Jumatano.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 29 aliambia ESPN nchini Mexico: Sijatia saini makubaliano yoyote kufikia sasa kwa sababu bado tunaendelea kujadiliana.

Alipoulizwa kuhusu pigano hilo kufanyika Saudia alisema: Wanataka kuliandaa huko lakini lazima tuone pale tutakapojadiliana na timu yangu. Ningependa pigano hilo kufanyika tena New York.

Ruiz alimshinda Joshua ambaye alikuwa anapigiwa upatu kushinda pigano hilo kwa urahisi katika ukumbi wa Madison Square Garden mjini New York tarehe 1 mwezi Juni.

Baada ya kupata ushindi alichukua mataji ya IBF WBA na WBO na kuwa raia wa kwanza wa Mexico kushinda mataji katika uzani huo.

Joshua alitumia haki yake ya kutaka pigano la marudiano na promota Eddie Hearn amesisitiza kuwa Ruiz ni sharti atie saini makubaliano hayo kwa kuwa ni miongoni mwa mkataba wa pigano la kwanza.

Hearn amesema kuwa timu ya Joshua inafaa kumjuza Ruiz wakati, tarehe na ukumbi wa pigano hilo na kwamba huenda bingwa huyo akakabiliwa kisheria iwapo pigano hilo halitafanyika.

Waandalizi wa pigano hilo nchini Saudia wamewekeza kitita cha $40m (£33m) kuandaa pigano hilo lakini kumekuwa na ukosoaji mkubwa wa kupeleka pigano hilo eneo kama hilo ambalo linadaiwa kuwa na rekodi mbaya ya haki za kibinadamu .

Shirika la Amnesty International limesema kuwa hatua hiyo inatoa fursa kwa mamlaka ya Saudia kusafisha rekodi yake mbaya kupitia michezo.