- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BIFU LA DIAMOND NA CLOUDS MEDIA LIMEKWISHA HII LEO
Uhasama uliokuwepo kwa muda mrefu baina ya Mkurugenzi wa Wasafi Media Naseeb Abdul Maarufu kama Diamond Platnumz na uongozi wa Clouds Media Group unaweza sema umekwisha mara baada ya Wimbo wa Diamond kupigwa hii leo kwenye Radio ya CloudsFm katika kipindi cha Power breakfast.
Hatuo hiyo imekuja hii leo Aprili 4, 2020 wakati Mkrungenzi mtendaji na CEO wa Clouds Media Group JosephKusaga kuzindua kampeni ya BONGE LA MPAMBANAJI ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi corona.
Wakati akihojiwa na Power Breakfast ya CloudsFM Kusaga akasema anao Wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na DiamondPlatnumz ambaye alimpigia simu LIVE na kuzungumza kwenye Power Breakfast.
Akiongea kwenye PB Diamond amesema “Kwanza nimpongeze CEO Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”
Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe Msanii wake mpya Zuchu lakini baada ya Jo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa.