- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BIBI KIKONGWE AJIFUNGUA MAPACHA WAWILI
Katika hali isiyoyakawaida kuna Mwanamke mmoja Mzee nchini India mwenye umri wa miaka 73 katika jimbo la Andhra Pradesh amejifungua watoto 2 mapacha wa kike, huku mumewe akiwa na umri wa miaka 82 kwa njia ya kupandikiziwa yaani IVF.
Madaktari waliomsaidia kujifungua mapacha hao wanasema amejifungua kwa njia ya kuanguliwa kwa mayai yake ya uzazi nje ya mfuko wa uzazi na baadae kuchanganywa na mbegu za kiume na kisha kupandikizwa ndani ya mfuko wake wa uzazi ama IVF kwa lugha ya kitaalamu. Alipatiwa kwanza matibabu ya IVF, Siku ya Alhamisi.
"Mama na watoto kwa pamoja wanaendelea vizuri,"Dkt. Uma Sankar amekiambia kituo cha habari cha BBC.
Mangayamma Yaramati amesema yeye na mumewe ambaye ana umri wa miaka 82, wamekuwa wakati wote wakutaka kuwa na watoto lakini hawakuwahi kupata mtoto hadi sasa.
"Tumefurahi sana ,"mesema mume wake, Sitarama Rajarao, akiongeza kuwa mkewe alipata ujauzito katika kipindi cha miezi miwili tu baada ya kufanyiwa matibabu ya IVF.
"Tulijaribu mara nyingi kupata watoto na tukawatembelea madaktari wengi ," Amesema Bi Yaramati , "kwa hiyo hiki ni kipindi cha furaha zaidi maishani mwangu ."
Aliongeza kuwa alihisi kutengwa na jamii na wanakijiji wenzake na mara kwa mara amekuwa akitengwa katika mikusanyiko kwasababu yeye hakuwa mama.
Anasema :"walikuwa wananiita mwanamke asiye na mtoto ,"
Lakini siku ambayo watoto wake mapacha walipozaliwa, Bwana Rajarao alipata kiharusi. Kwa sasa anapokea matibabu hospitalini.
Mapacha hao wasichana walizaliwa kwa njia ya upasuaji , jambo ambalo ni la kawaida kwa uzazi huo wa nadra.