- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BIASHARA YA NYAMA YANGURUWE YAPIGWA STOP DODOMA
DODOMA: HALMASHAURI ya manispaa ya Dodoma imetangaza rasmi zuio la kutokufanya biashara ya nguruwe na mazao yake kuanzia sasa mpaka itakapotangazwa,kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe katika wilaya ya Dodoma .
Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini ,CHRISTINA MNDEME katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa BI.MNDEME amebainisha kuwa halmashauri ya manispaa ya Dodoma kwa mamlaka iliyonayo kwa sheria ya magonjwa ya mifugo namba 17 ya mwaka 2003,kifungu cha 15,imetangaza rasmi kuwepo kwa ugonjwa huo wa nguruwe kwani mpaka sasa nguruwe zaidi ya 200 wamekufa katika kata ya miyuji na wengine 85 wamekufa katika kata ya ipagala iliyopo wilayani humo .
kufuatia kuwepo kwa hali hiyo,amesema mnyama yeyote wa jamii ya nguruwe (ngiri,nguruwe pori,au nguruwe wa kufugwa ) hawataruhusiwa kutoka au kuingia katika wilaya ya Dodoma bila kibali maalum cha maandishi kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma.
aidha amesema bidhaa yoyote inayotokana na mnyama jamii ya nguruwe,ikiwemo mbolea,kinyesi,mkojo na damu haziruhusiwi kusafirishwa,kuingizwa au kutolewa nje ya wilaya ya Dodoma pasipo kibali maalum cha maandishi kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma.