Dkt Kijo Bisimba ameyabainisha hayo leo Aprili 5, 2020 wakati akifanyiwa mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha EATV na East Africa Radio na kusema kuwa kwa sasa anafurahia maisha ya kustaafu kwa sababu yanampa nafasi yakupanga muda wa majukumu yake kwa siku.
"Mwenzangu hilo jina hapana mimi siyo kigogo na ukiangalia kwenye mitandao kuna mtu anaitwa kigogo, wasije wakanifananisha naye, mimi ni Mama na kitaaluma mimi ni Dkt" amesema Dkt Kijo Bisimba.
Kigogo amekuwa mkosoaji mkubwa katika Serekali hii ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Amekuwa akielekeza mambo ambayo serekali inapaswa kufanya na mambo ambayo yanaenda kombo Serekalini.
Novemba 2, mwaka jana Aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Kangi Lugola aliahidi kumkamata Mtu huyo(Kigogo) huku akisema kuwa siku zake zinahesabika.
Lakini Mnamo Januari 23, 2020 aliondolewa katika baraza la Mawaziri mara baada ya Rais Magufuli kumtuhumu Waziri huyo kuhusika katika Mkataba wa kifisadi.
Rais Magufuli alisema kasoro iliyofanyika katika mkataba huo akimhusisha aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na Lugola aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Magufuli alieleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za maofisa wa Jeshi la Magereza, Ukonga Dar es Salaam, kueleza kuwa Lugola na Andengeye wamefanya mambo mazuri lakini kutokana na kasoro hizo za mikataba, hawafai kuendelea na nyadhifa zao.
Baadaye mchana Balozi Kijazi alisoma mabadiliko yaliyofanywa na Magufuli aliyemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Katika hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo, Lugola aliwataka Watanzania kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.