- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BENKI KUU YASEMA NOTE YA TZ HAIWEZI KUBAKI NA CORONA
Benki Kuu ya Tanzania Imesema kuwa Note za Tanzania haziwezi kubeba aina yeyote ya vimelea, vikiwemo virusi vya Corona vinavyotishia Dunia kwa Sasa.
Hata hivyo Katika taarifa yake ya BOT iliyotolewa leo Machi 19, 2020, BOT imewashauri watanzania kutumia njia mbadala katika kufanya miamala kwa njia za kieletroniki kama ATM, na njia zingine za Inteneti.
“Noti zetu zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti, hata hivyo kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, tunawashauri Wananchi kuzingatia miongozo ya kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au sanitizer”-Benki Kuu ya Tanzania (BOT)"
“Katika kipindi hiki ambacho tuna janga la corona, tunawashauri Wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti”-BOT
“Corona ni tishio Duniani kote na tayari Tanzania tuna wagonjwa watatu, tunawasihi Wananchi katika kipindi hiki ambacho Taifa linapambana na corona kuzipuuza taarifa zinazozagaa mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika, zinazozihusisha noti zetu na usambazaji wa corona” - BOT