- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BEI YA MAFUTA YAPANDA DUNIANI BAADA YA VIKWAZO VYA IRANI
Uamuzi wa serikali ya rais wa Marekani Donald Trump wa kuziwekea vikwazo nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran umeibua wasiwasi kuhusu usambazaji wa kimataifa wa mafuta ghafi, huku bei ya mafuta ikipanda kwa kiasi kikubwa tangu mwezi Oktoba.
Wataalamu wa sekta hiyo wamesema jana kuwa vikwazo hivyo vinaweza kupelekea kupungua kwa hadi mapipa milioni 1.2 ya mafuta katika soko la kimataifa. Lakini idadi hiyo inaweza ikawa ndogo zaidi kulingana na jinsi nchi zitakavyoupokea uamuzi huo wa Marekani na kiasi cha mafuta ambacho Iran itaendelea kusafirisha.
Rais Trump amesema anataka kuvuruga mapato ya Iran yanayotokana na mauzo ya mafuta. Trump anaamini fedha hizo zinatumiwa na Iran kufadhili shughuli ambazo ni za uharibifu katika Mashariki ya Kati na kwengineko.