Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:34 am

NEWS: BAVICHA WATINGA KWA IGP SIRRO NA BARUA KULAANI VITENDO VYA UNYANYASAJI VINAVYOFANYWA NA JESHI LA POLISI

DAR ES SALAAM: Baraza la vijana chadema [BAVICHA] wameandika barua kwenda kwa Mkuu wa jeshi la polisi [IGP] Simon Sirro na Mkurungezi wa makosa ya ya jinai[DCI] Robert Boaz kwa kulitaka jeshi la polisi lijibu na kufanyia kazi malalamiko yao ya kuchoshwa na matendo maovu na machafu yaliyo kinyume na katiba ,sheria,taratibu na kanuni zauendeshwaji wa vyombo vyenye mamlaka za kidola kama nchi huru.

Lakini pia barua hiyo imeelezajuu ya uvunjaji wa sheria , matumizi mabaya ya mamlaka , ubambikizwaji kesi,ukiukwaji na haki za binadamu , demokrasia na utawala bora unaofanywa na watendaji wa jeshihilo’’

Barua hiyo iliendelea kueleza vitendo vya unyanyasaji huounawalenga wanasiasa wa vyama vya upinzani na wafuasi enforcement ]. Wameitaka ofisi ya IGP kwa mujibu wa sheria itekeleze yafuatayo.

A]Iwaeleze watanzania kwanini na kwa sheria ipi ya jeshi nla polisi linazuia vyama vya vya siasa vya upinzani ususani CHADEMA Kutekeleza hakli kwa wajibu wake wa kikatiba na sheria ikiwemo kukutana, nakujenga chama cha kufanya mikutano ya hadhara.

B] Iwaeleze watanzania kuwa siasa za upinzani ni kosa la jinaina kama sivyo kwanini jeshi la polisi kwa matendo na kauli [ushahidi upo] linaonekana mstari wa mbele kupambana na upinzani zaidi na kuwakingia kifua wana CCM vishindane kwa sera , hoja na mawazo yatakayolisaidia Taifa.

C] Jeshiletu linapolalamikiwa kila mara na kutuhumiwa kuwa na upendeleo ‘’Double standards and bias’’ hawaoni ni hatari kwa usalama wa nchi yetu siku za mbeleni.

Barua hiyo ilipelekwa ofisini kwa IGP na DCI jana Saa 8: 32 mchana na mwenyekiti wa baraza la vijana Taifa, Patobass Katambi,Akiongozana na katibu wa baraza hilo Peter Mwita

BAVICHA kupitia mtandao wa instagramwaliendelea kusisitiza kuwa kama barua yao haitajibiwa wala kuchukuliwa hatua zozote baraza hilo litaratibumaandamano ya amani nchi nzima mnamo tarehe 31/8/2017 mwaka huu.